VIRUTUBISHO VINAVYOPATIKANA KATIKA NYAMA NYEKUNDU
Imewekwa: 12 Apr, 2023

Nyama nyekundu ni chanzo cha virutubisho muhimu (virutubisho ambvyo vinapatiakana tu kwenye chakula, ambavyo mwili hauwezi kujitengenezea) ambavyo vinatakiwa kwa afya na ukuaji mzuri.

Hapa chini tutaelezea baadhi ya virutubisho vinavopatikana katika nyama nyekundu:

  • PROTINI: Nyama nyekundu ni chanzo kizuri cha protini yenye ubora wa hali ya juu, amabyo ni muhimu kwa kujenga mwili na kutengeneza tishu za misuli zilizoharibika.
  • MADINI YA CHUMA: nyama nyekundu ni chanzo kizuri kwa virutubisho lishe vya madini ya chuma. Madini ya chuma muhimu kwa uzalishaji wa chembe nyrkundu za damu na kusafirisha hewa ya oksijeni katika mwili.
  • VITAMINI B12: nyama nyekundu ni moja ya vyanzo adimu vyenye vitamini B12, ambavyo muhimu kwa uzalishaji wa chembe nyekundu za damu, ufanyaji kazi kwa usahishi mfumo wa neva na uzalishaji wa vinasaba (DNA).
  • ZINKI: nyama nyekundu ni muhimu kama chanzo cha zinki ambayo ni muhimu kwa ufanyaji kazi wa kinga ya mwili, kuponesha madonda na uzalishaji wa vinasaba (DNA).
  • SELENIUMU: nyama nyekundu ni chanzo kizuri cha madini ya seleniamu ambayo ni muhimu kwa ufanyaji kazi wa tezi ya thairoidi, ufanyaji kazi kinga ya mwili  na ulinzi wa antioxidant.
  • NIASINI: nyam nyekundu chanzo kizuri cha niasini ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa nishati ya mwili, kurekebisha chembe za vinasaba na ufanyaji kazi wa mfumo wa neva.
  • PHOSPHORASI: nyama nyekundu ni chanzo cha madini ya phosforasi ambayo ni muhimu kwa afya ya mifupa, uzalishaji wa nishati ya mwili na uzalishaji wa vinasaba.

Angalizo, ni muhimu kuzingatia kuwa mikato mbali mbali ya nyama nyekundu inatofautiana katika viwango vya virutubisho vilivyopo, ni muhimu kuchagua mikato isiyo na mafuta na kuwa na kiasi katika ulaji wa nyama hivyo kuepuka kiwango kikubwa cha mafuta yanayoganda mwilini na kiwango kikubwa cha lehemu. Kwa kuongezea, ni muhimu kupika nyama kwa usahihi na kuivaa vizuri kuhakikisha usalama wa chakula na kuzuia uwepo/kutokea kwa vimela hatarishi vinavyoweza kuongezeka kwa magonjwa sugu.