Bodi ya Wakurugenzi

Bodi itaundwa na Mwenyekiti na wajumbe wengine walioteuliwa na Waziri kama ifuatavyo:

(a) mjumbe mmoja anayewakilisha Wizara yenye dhamana na Mifugo;

(b) mjumbe mmoja anayewakilisha Wizara yenye dhamana na Serikali za mitaa;

(c) mjumbe mmoja anayewakilisha taasisi yenye dhamana ya udhibiti ubora wa vyakula;

(d) mjumbe mmoja anayewakilisha taasisi zenye dhamana ya kufanya utafiti katika maendeleo ya tasnia ya nyama;

(e) mjumbe mmoja mwenye elimu ya uchumi kilimo; na

(f) wajumbe watatu kutoka sekta binafsi.