Majukumu ya Bodi

Majukumu ya Bodi ya Nyama yameainishwa katika Kifungu Na. 10 (a – w) cha Sheria ya Nyama Na. 10 ya Mwaka 2006.

Majukumu hayo yamegawanyika katika mafungu makuu manne kama yalivyoorodheshwa hapa;

1. Kuhamasisha, kusimamia na kuratibu shughuli za maendeleo ya tasnia ya nyama.

  • Kuandaa, kutekeleza na kusimamia mpango mkakati wa kuendeleza tasnia ya nyama
  • Kuhamasisha uzalishaji kwa kutumia teknolojia sahihi ili kuzalisha nyama bora itakayokidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi
  • Kukusanya, kuchambua, kuhifadhi na kusambaza taarifa na takwimu muhimu zitakazosaidia kuboresha, au kuongeza uzalishaji, uwekezaji, usindikaji na masoko
  • Kuhamasisha uundaji na uimarishaji wa vikundi na vyama vya wadau katika tasnia ya nyama

2. Kuendeleza sekta na kusimamia ubora wa mifugo, nyama na mazao yake.

  • Kwa kushirikiana na Taasisi zinazohusika na udhibiti wa ubora, kudhibiti ubora wa viwango vya uzalishaji wa mifugo, nyama na mazao yake kwa mujibu wa Sheria ya Nyama Na. 10 ya Mwaka 2006 na kanuni zake

3. Kutafuta, kuendeleza na kufuatilia masoko ya mifugo, nyama na bidhaa zake ndani na nje ya nchi.

  • Kujenga uwezo wa ushindani wa kibiashara miongoni mwa wadau wa tasnia ya nyama
  • Kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara, kufanya utafiti wa Masoko ya Mifugo, Nyama na bidhaa zake na kuyaendeleza
  • Kusimamia na kufuatilia mikataba ya masoko kati ya wazalishaji na wafanyabiashara, wasindikaji na kusuluhisha pale inapotekea kutokuelewana baina ya pande hizo

4. Kufanya ushawishi na utetezi wa wadau wa tasnia ya nyama.