Masoko

Masoko

UTARATIBU WA KUFANYABIASHARA YA KUUZA NYAMA NJE YA NCHI (EXPORT) NA KUINGIZA BIDHAA ZA NYAMA NCHINI (IMPORT)

1.0       Hatua ya Kwanza (Kusajiliwa na Bodi ya Nyama Tanzania)

1.1       Nani anahitajika Kusajiliwa?

Kampuni/ kikundi/ mtu binafsi ambaye atakuwa anazalisha nyama na bidhaa za nyama kwa ajili ya kuuza katika soko la nje ya nchi (Meat & Meat Products Exporters). Pia Kampuni/Kikundi/mtu binafsi ambaye atakuwa anafanya biashara ya kuingiza nyama na bidhaa za nyama ndani ya nchi (Meat & Meat products importers)

1.2       Faida za Kusajiliwa ni zipi?

  1. Kuipatia utu wa kisheria biashara yako
  2. Kutambulika na taasisi/mamlaka mbalimbali zinazosimamia biashara.
  3. Kuwahakikishia watumiaji wa bidhaa zako ubora na usalama wa bidhaa husika
  4. Kuzisaidia mamlaka husika kupata takwimu sahihi za biashara husika

1.3       Taratibu na Mahitaji wa Kusajiliwa kwa Mfanyabiashara wa kupeleka nyama na bidhaa nje ya nchi (exporters)

1.3.1    Nyaraka za Kuwasilisha

  1. Namba ya Utambulisho ya Mlipaji Kodi (TIN) 
  2. Picha (passport size)
  1. Kitambulisho cha NIDA/Leseni/Mpiga kura
  1. Kama ni Kampuni/kikundi/taasisi ambatisha cheti cha usajili wa kampuni/kikundi/taasisi

1.3.2    Hatua 4 za kufuata ili kujisajili

  1. Kujaza fomu ya maombi kupitia ; https://mimi.mifugo.go.tz au link hiyo kupitia www.tmb.go.tz
  2. Kuambatisha nyaraka husika
  3. Kukamilisha Malipo kupitia mfumo
  4. Kurudufu (print) cheti za Usajili

Ada ya Usajili ni shilingi 70,000, pia uhai wa usajili ni mwaka mmoja (Julai – Juni)

Kila mdau anapaswa kuhuisha udau wake kila mwaka wa fedha unapoanza

1.4 Taratibu na Mahitaji wa Kusajiliwa kwa Mfanyabiashara wa kuingiza nyama na bidhaa za nyama nchi (importers)

1.4.1 Nyaraka za Kuwasilisha

  1. Namba ya Utambulisho ya Mlipaji Kodi (TIN) 
  2. Picha (passport size)
  1. Kitambulisho cha NIDA/Leseni/Mpiga kura
  1. Kama ni Kampuni/kikundi/taasisi ambatisha cheti cha usajili wa kampuni/kikundi/taasisi

1.4.2    Hatua 4 za kufuata ili kujisajili

  1. Kujaza fomu ya maombi kupitia ; https://mimi.mifugo.go.tz au link hiyo kupitia www.tmb.go.tz
  2. Kuambatisha nyaraka husika
  3. Kukamilisha Malipo kupitia mfumo
  4. Kurudufu (print) cheti za Usajili

Ada ya Usajili ni shilingi 70,000, pia uhai wa usajili ni mwaka mmoja (Julai – Juni)

Kila mdau anapaswa kuhuisha udau wake kila mwaka wa fedha unapoanza

2.0       Hatua ya Pili (Kupata Vibali vya kupeleka/kuingiza nyama na bidhaa za nyama (export clearance export)

2.1 Nyaraka za Kuwasilisha ili Kupata kibali cha kuuza nyama nje ( export clearance certificate)

  1. Usajili wa Bodi ya Nyama
  2. Leseni ya Biashara kutoka BRELA au Mamlaka nyingine zinazotoa leseni
  3. Hati/ankara ya madai (Invoice)
  4. Kibali cha kuingiza nyama kutoka nchi inakopelekwa (import permit)
  5. Orodha ya bidhaa (packing list)

2.2 Hatua 4 za kufuata kuomba kibali cha kupeleka nyama nje ya nchi (export)

  1. Kujaza fomu ya maombi kupitia mfumo wa mimis.mifugo.go.tz
  2. Kuambatisha nyaraka husika
  3. Kukamilisha Malipo kupitia - https://mimi.mifugo.go.tz au www.tmb.go.tz
  4. Kurudufu (ku print) kibali

Tozo ya kupeleka nyama nje ya nchi ni shilingi 70,000 kwa mzigo na kinadumu kwa siku 14

2.3 Nyaraka za Kuwasilisha ili Kupata kibali cha kuingiza (import clearance certificate)

  1. Usajili wa Bodi ya Nyama
  2. Leseni ya Biashara kutoka BRELA au mamlaka nyingine za leseni
  3. Invoice
  4. Kibali cha kutoa nyama kutoka nchi inapotoka (export permit)
  5. Orodha ya aina ya nyama/ bidhaa za nyama zinazoingizwa (Packing list)

2.4 Hatua za kufuata kupata kibali cha kuingiza nyama na bidhaa zake nchini (import clearance certificates)

  1. Kujaza fomu ya maombi kupitia https://mimi.mifugo.go.tzau www.tmb.go.tz
  2. Kuambatisha nyaraka husika
  3. Kukamilisha Malipo kupitia ;mimis.mifugo.go.tz
  4.  Kurudufu (print) kibali (clearance certificate)

Tozo ya kuingiza nyama na bidhaa za nyama nchini ni asilimia mbili (2%) ya thamani ya mzigo