TAARIFA YA ULIPIAJI WA HUDUMA ZITOLEWAZO NA BODI YA NYAMA
Imewekwa: 09 May, 2023

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA YA ULIPIAJI WA HUDUMA ZITOLEWAZO NA BODI YA NYAMA

Dodoma, 09 Mei, 2023

Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) inapenda kuwakumbusha wananchi  wote kuwa, malipo ya huduma zote zitolewazo na Bodi ya Nyama Tanzania ikiwemo Usajili wa Wadau, Uhuishaji wa kazi za Wadau (Retention), Utoaji wa vibali vya kuuza/kuingiza nyama na bidhaa za nyama n.k  yanafanyika kwa kutumia namba ya udhibiti wa malipo (control number) na sio pesa taslimu.

Vilevile, TMB inawakumbusha wadau wote kuwa itakapohitaji huduma kutoka ofisi yoyote ya Umma au Binafsi yenye gharama ya kulipia, malipo ya huduma hiyo yatafanyika kupitia akaunti ya Benki ya muhusika.

TMB inawashukuru wananchi na wadau wetu wote kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa. Aidha TMB inapenda kuwakumbusha kuwa endapo utakutana na kiashiria chochote cha utapeli usisite kuwasiliana na Bodi ya Nyama Tanzania kupitia namba 0734 996218 au barua pepe: barua@tmb.go.tz.

 

Imetolewa na:

BODI YA NYAMA TANZANIA