AINA YA MIKATO YA NYAMA
Imewekwa: 12 Apr, 2023

 

Mnyama aliyekwisha chinjwa (chune) anaweza kukatwa katika mikato (vipande) tofauti kulingana na ladha, ulaini. Hapa chini tutaelezea mikato tofauti maarufu ya chune:

  1. JEMBE:  hii ni yama inayopatikana eneo la shingo mwa mnyama, ni nzuri kwa mapishi ya taratibu (muda mrefu) kama vile mchemsho au mchuzi. Ni nyama au mkato mgumu na inakuwa laini endapo ikipikwa kwa muda mrefu.
  2. MBAVU:  ni mkato wa nyama inyopatikana nyuma ya shingo, inafahamika haswa kwa ung’aavu, ulaini na ladha nzuri
  3. SALALA: aina hii ya mkato inapatikana katikati mwa mgongo wa mnyama na inajumuisha baadhi ya mikato milaini na ladha nzuri kama vile mkato-T
  4. KIUNO: ni nyama inayopatikana nyuma ya chune ya mnyama na inafahamika kwa ladha kali inaweza kupikwa kwa kuchomwa kwenye moto mkali na mdogo, mara kwa mara inapikwa kwa kukangwa na mchuzi
  5. PAJA: huu mkato unapatikana mguu wa nyuma wa mnyama, ni mkato usiokuwa na mafuta ni nyama nzuri kwa mapishi ya taratibu (moto mdogo) kama vile kuchoma kwenye moto mdogo.
  6. KIDALI: huu mkato wa nyama unaopatikana kifuani ni ngumu, yenye ladhani nzuri kwa kufukizwa moshi au mapishi ya taratibu
  7. TUMBO: huu ni mkato wa nyama inayopatikana maeno ya tumbo la mnyama, ni nyama isiyo na mafuta yenye ladha ni nzuri kwa kuchomwa kwenye moto, kuoka na kuachwa kwenye viungo.
  8. MBAVU LAINI/ MBAVU FUPI: mkato huu upo kwenye tumbo la mbele la ng'ombe na hutumiwa kusaga na nyama ya mchuzi

Hizi mikato michache maarufu ya nyama, na kila moja una ubora wake wa kipekee na matumizi yake.