HASARA YA KUGANDISHA TENA NYAMA ILIYOKWISHA YEYUSHWA
Imewekwa: 12 Apr, 2023

Kurudia kugandisha nyama iliyokwisha yeyushwa inaweza kuwa na hasara nyingi, zikijumuisha:

  1. Kupungua kwa ubora: kugandisha tena nyama matokeo yake ni kupungua kwa ubora, chembe chembe za barafu zililzojitengeneza mara ya kwanza inaweza kuharibu ladha na mguso wa nyama. Hii itsababisha nyama kuwa ngumu, kavu  na isiyo na ladha
  2. Kuongezeka hatari ya kukua kwa vimelea vya bakteria: nyama  inapokua inayeyushwa, bakteria wanaweza kuanza hatua za ukuaji kwa haraka juu ya nyama. Kuigandisha tena hii nyama inasababisha kuongezeka maradufu, hivyo basi kuongezeka kwa hatari ya magonjwa yatokanayo na vyakula.
  3. Kuunguzwa ndani ya jokofu: kugandisha tena kwa nyama kunaweza kusababisha kupoteza kwa unyevu unyevu wa nyama hii hutokea kwa kuungua kutokana na ubaridi, hii hutokana na hewa ndani ya jokofu endapo itawekwa kwa muda mrefu.
  4. Kupungua kwa muda wa kutunzwa: nyama iliyoyeyushwa na kugandishwwa tena inakua na muda mfupi kwa kutunzwa hivo kupelekea kuharibika kwa haraka hivyo kutokufaa kwa matumizi.

Kuepukana na haya, njia bora ni kuyeyusha kiasi kidogo unachopanga kutumia kwa mapishi na kupika mara tu baada ya kuyeyuka. Na kama umeyeyusha kiasi kikubwa nje ya mpango, ni bora kuipika yote na kuhifadhi nyama iliyopikwa.