TOFAUTI KATI YA NYAMA NYEUPE NA NYAMA NYEKUNDU
Imewekwa: 12 Apr, 2023

Nyama nyekundu na nyama nyeupe ni aina mbili tofauti za nyama zinazotoka katika vyanzo tofauti na zina utofauti wa kipekee wa uwepo wa virutubisho lishe.

Nyama nyekundu zinapatikana kwa mamalia na inajumuisha nguruwe, kondoo, mbuzi. Nyama inamuonekano wa rangi nyekundu kutokana na uwepo wa protini za chembe chembe nyekundu zijulikanazo kama myoglobini, zinzotumika kuhifadhi hewa ya oksijeni katika tishu za misuli. Nyama nyekundu ni nyama yenye kiwango kikubwa cha mafuta na ina kiwango kikubwa cha myoglobini zaidi ya nyama nyeupe. Na pia chanzo kizuri cha virutubisho muhimu vya madini na vitamini kama vile chuma, zinki na vitamini B12.

Nyama nyeupe chanzo chake ni wanyama jamii ya ndege kama vile kuku, bata mzinga na bata. Nyama hii nyeupe inaonekana na uweupe ng’aavu inatokana na uchache wa chembe chembe nyekundu za myoglobini ukilinganisha na nyama nyekundu. Nyama nyeupe kwa kawaida ina kiwango kidogo cha mafuta kulinganisha na nyekundu. Ni chanzo kizuri cha protein yenye mafuta kidogo na ina virutubisho muhimu kama vile nasini, vitamini B6 na seleniamu.

Kwa ujumla wake, nyama nyeupe na nyama nyekundu kwa kiasi fulani zinatoa faida tofauti za lishe  na inaweza kujumuishwa katika lishe yenye afya kwa kiasi. Inapendekezwa kutumia mikato ya nyama isiyo na mafuta kwa aina zote mbili za nyama na kuweka uwiano sawa wa matumizi ya nyama na aina nyingine za vyanzo vya protini kama vile samaki, maharage na jamii za mikunde. Kwa kuongezea, ni muhimu kupika nyama kwa usahihi na kuivaa vizuri kuhakikisha usalama wa chakula na kuzuia wepo/kutokea kwa vimelea hatarishi vinavyoweza kuongezeka kwa magonjwa sugu.