USHAURI WA ULAJI WA NYAMA KWA KUZINGATIA MAKUNDI YA UMRI (WATOTO, VIJANA NA WATU WAZIMA)
Imewekwa: 12 Apr, 2023

1. WATOTO: watoto wanahitaji mlo uliokamili unaojumuisha virutubisho mbalimbali kwa ukuaji na maendeleo. Ni muhimu kuchagua mikato isiyo na mafuta na kuondoa mafuta yote yanayoonekana. Madaktari wa watoto kutoka chuo cha amerika wanashauri mtoto mwenye mwaka 1 hadi mitatu (1-3) kula nyama isiyozidi gramu 28 kwa siku wakati watoto wenye umri kuanzia miaka 4-8 wanaweza kula mpaka gramu 42.5 kwa siku.

 

2. VIJANA: wenye umri kuanzia 13 hadi 19 na wenye umri kati ya 18-25 wana uhitaji mkubwa wa nishati mwilini na wanaweza kuhitaji virutubisho vya protini zaidi. Nyama isiyo na mafuta ni chanzo kizuri cha protini, chuma na virutubisho vingine muhimu. Shirika la Moyo Marekani linapendekeza kwamba watu wazima walio na umri wa miaka 18 na zaidi wasitumie zaidi ya gramu 170  za nyama iliyopikwa isiyo na mafuta, kuku, au samaki kwa siku.

 

3. WATU WAZIMA:  kadiri umri unavyoenda wa mtu, mahitaji ya lishe yanaweza kubadilika na wanaweza kuhitaji karoli chache lakini protini kwa wingi kudumisha idadi na uimara misuli. Watu wenye umri mkubwa wanaweza kuwa na shida ama kupata shida ya kumeng’enya baadhi ya chakula, hivyo ni vizuri kuchagua nyama isiyo na mafuta na kuepuka nyama iliyosindikwa/kuchakatwa. Chuo cha lishe na milo wanapendekeza watu wenye umri mkubwa kutumia gramu 1-1.2 ya protini kwa uzito wa mtu kwa siku.

 

Ni muhimu kuzingatia kuwa kila mmoja ana mahitaji yake maalumu ya kiafyaa au kilishe ambayo inaweza kuathiri uwezo wake wa kutumia aina fulani ya nyama au mikato ya nyama. Ni vema mara zote kuomba ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya au wataalamu wa lishe waliosajiliwa.