Karibu

Wapendwa,

 

Tunafurahi kuwakaribisha wote kutembelea Tovuti ya Bodi ya Nyama Tanzania. Tovuti hii itakuhabarisha kuhusu kazi za Bodi, matarajio na hamasa yetu katika kuendeleza tasnia ya nyama. Tovuti itakupa taarifa muhimu ambazo ni pamoja na dira, dhima, majukumu, huduma, habari na matukio mbali mbali ya Bodi na tasnia kwa ujumla. Tuko mstari wa mbele kukupa huduma zenye ubora pamoja na kukuwezesha kupata nyama na bidhaa zake bora na salama kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi. Tunakushukuru kwa kupata nafasi ya kutembelea tovuti yetu na nimatumaini yetu kwamba utafurahia kupata taarifa mbalimbali na zimekusaidia.

Nyama Bora na Salama kwa wote !!!

Karibu