Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) imeendelea kutoa elimu kuhusu tasnia ya nyama na ufanyaji wa biashara ya nyama kwa wananchi katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma mwaka 2026.
Akizungumza na wananchi waliotembelea banda hilo Afisa Mkaguzi kutoka TMB Bw. Alex Mkenda amesema Bodi hiyo inaendelea kufanya usajili wa wadau wa bucha na machinjio wanaofika katika banda hilo na ofisini pia wanahamasisha wadau kutembelea bandahilo ili kujionea bidhaa za wadau hasa Mdau Happy Soseji ambae ameshiriki kwenye maonesho hayo
Bw. Mkenda amesema “wananchi waje kutembelea banda la TMB ili kupata elimu na kuonja bidhaa ya soseji ambayo inazalishwa na mdau wetu Happy soseji tunayeshirikiana nae katika maonesho haya”.
Aidha Bw. Mkenda amewahamasisha wadau wa tasnia ya nyama kufanya uhuishaji wa udau wao kwa mwaka 2026/2027 ambao utaanza rasmi Julai 1 hadi 30 ili kuepuka penati ambayo itaanza Agosti 1 kwa watakaochelewa kuhuisha.
Bodi ya nyama itakuwepo katika maadhimisho hayo na kutoa huduma zake hadi Juni 23 yatakapohitimishwa rasmi.

