Imewekwa: 08 Apr, 2024

Bei ya wastani ya mifugo katika mnada wa Pugu imeshuka kidogo ikilinganishwa na wiki iliyopita, kwa kiasi kikubwa hali hiyo imesababishwa na kupungua kwa uhitaji wa mifugo mnadani lakini pia hali hii inachangiwa na wafugaji kutokupeleka mifugo mizuri kwa wingi wakisubiri mpaka kipindi cha sikukuu ya Eid.