Imewekwa: 14 Jan, 2026
Bei ya wastani ya mifugo katika mnada wa Pugu imepanda kwa wiki inayoishia tarehe 25 Desemba 2025 ikilinganishwa na wiki iliyopita. Kwa kiasi kikubwa hali hiyo imesababishwa na kupungua kwa ugavi wa mifugo mnadani, huku uhitaji ukiwa ni mkubwa kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

