Imewekwa: 19 Nov, 2024
Bei ya wastani ya mifugo hasa ng’ombe katika mnada wa Pugu inaonekana kupanda kidogo ikilinganishwa na wiki iliyopita, sababu kubwa ikiwa ni kupungua kwa ugavi wa ng’ombe mnadani. Huku bei ya wastani ya mbuzi na kondoo inaonekana kutobadilika ikilinganishwa na wiki iliyopita, kutokana na hali ya soko kubaki kawaida.