Mwenendo wa bei ya wastani ya mifugo katika mnada wa Pugu kwa wiki inayoishia tarehe 07 Juni 2024
Imewekwa: 12 Jun, 2024
Mwenendo wa bei ya wastani ya mifugo katika mnada wa Pugu kwa wiki inayoishia tarehe 07 Juni 2024

Bei ya wastani ya mifugo katika mnada wa Pugu kwa wiki inayoishia tarehe 07 Juni 2024 imepanda kidogo ikilinganishwa na wiki iliyopita, kwa kiasi kikubwa hali hiyo imesababishwa na wafugaji kutopeleka mifugo mnadani kwa wingi wakisubiri kufanya hivyo katika kipindi cha sikukuu ya Eid Al Adha.