Imewekwa: 08 Apr, 2024

Bei ya wastani ya mifugo ( ng’ombe na mbuzi ) katika mnada wa Pugu imeshuka kidogo ikilinganishwa na wiki iliyopita, kwa kiasi kikubwa hali hiyo imesababishwa na kupungua kwa uhitaji wa mifugo mnadani na wafugaji kutokupeleka mifugo mizuri kwa wingi wakisubiri mpaka kipindi cha sikukuu ya Iddi. Kwa upande wa kondoo, wastani wa bei imepanda kidogo ikilinganishwa na wiki iliyopita, hali hii imesababishwa na kupungua kwa ugavi wa kondoo mnadani huku uhitaji wa ukiwa ni mkubwa.