BODI YA NYAMA YAPONGEZWA NA WANANCHI KATIKA UTOAJI WA VIBALI
Imewekwa: 14 Aug, 2025
BODI YA NYAMA YAPONGEZWA NA WANANCHI KATIKA UTOAJI WA VIBALI

BODI YA NYAMA YAPONGEZWA NA WANANCHI KATIKA UTOAJI WA VIBALI

Bodi ya Nyama Tanzania yapata pongezi za utoaji wa vibali kwa wafanyabiashara ya nyama ikiwemo maduka ya nyama.

Pongezi hizo zimetolewa na wananchi waliofika katika maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma na kupata elimu juu ya shughuli zinazofanywa na bodi hiyo na namna bodi inavyosimamia miongozo katika biashara hiyo.

Wageni waliotembelea kwenye banda la bodi ya nyama wamefanikiwa kujua taratibu zinazotakiwa katika ufanyaji wa biashara ya nyama na wengi wao walitaka kufahamu kuhusu uuzaji wa nyama nje ya nchi ambapo wananchi hao walielekezwa taratibu za kufuata ili kuweza kupata kibali  cha uuzaji wa nyama nje ya nchi.

Katika maadhimisho hayo Bodi ya Nyama imeshiriki kwa kutoa elimu na kuuza bidhaa kupitia wadau wake akiwemo HUSAM, MIKA MEAT na Kili Agro. Bidhaa zilizouzwa na wadau ni pamoja na vifaa sahihi vinavyotumika kwenye maduka ya nyama na machinjio ikiwemo mashine za kukatia nyama, nondo, visu, mizani na friza. Pia kulikuwa na soseji  na nyama ya kuku.

Aidha, wananchi hao wameiomba bodi kuongeza ukaguzi wa nyama hasa maeneo ya vijijini kwani kumekuwa na uchnjaji holela na ambao unaweza kuhatarisha afya zao kutokana na mifugo inayochinjwa kutokuwa na sifa zinazotakiwa ikiwemo magonjwa.