Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wamekutana na kufanya kikao kazi cha kujadili rasimu ya pili ya mwongozo wa utoaji Sadaka na Qurban nchini ili kuwawezesha watoaji wa sadaka hizo kufuata taratibu zinazotakiwa kabla ya kuitoa .
Kikao hicho kimehusisha Maafisa kutoa Bodi ya Nyama Tanzania, Idara ya Huduma za Mifugo na Idara ya Uendelezaji wa masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, BAKWATA na kampuni ya MIHB iliyokasimishwa na BAKWATA kusimamia uchinjaji na wachinjaji nchini kwa mujibu wa taratibu za HALAL. Kikao hicho kimefanyika Septemba 20, 2024 jijini Dodoma.
Katika kikao hicho mambo kadhaa yaliyojadiliwa Katika mwongozo huo ikiwa ni pamoja na aina za wanyama, sifa wanazostahili kuwa nazo, taratibu za kufata kwa watoaji wa sadaka na Qurban kabla ya kutoa sadaka hizo
Vilevile, Bakwata imepewa jukumu la kutambua Mfadhaili au taasisi zote zinazotoa Sadaka na Qurbani na Kisha Kutambulisha Mfadhili/ Taasisi kwa MIHB ili kujiridhisha kama wahusika wamekidhi vigezo vya utoaji sadaka kabla ya kuwafikia wanufaika na kuwasilsha orodha yao kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Nakala Bodi ya Nyama kwa ajili ya taarifa i
Pia katika mwongozo huo imeelezea kwamba ili mtu aweze kutoa Sadaka au Qurban itakayolenga wanyama wengi zaidi ni lazima apitie kwenye taasisi zilizosajiliwa kwa jukumu hilo na sio kutoa kama mtu mmoja mmoja ili kuweza kufuatilia na kujiridhisa kama taratibu za ugawaji wa sadaka umefuatwa kama ulivyoelekezwa kwenye mwongozo ikiwemo kuzingatia Sheria ya ustawi wa wanyama Na. 2008 Sheria Sheria ya magonjwa ya wanyama sura ya 156 , Sheria ya Tasnia ya nyama sura ya 421 pamoja na Sheria nyingine zinazohusiana na Uchinjaji wa Mifugo na Uzalishaji wa nyama bora na salama Nchini na taratibu za ugawaji wa Sadaka na Qurbani
Wajumbe wa kikao hicho wamekubaliana kukutana tena Oktoba 16, 2024 ili kuweza kukamilisha mwongozo huo na kuanza kutumika baada ya kupitishwa rasmi.