UKAGUZI WA NYAMA BORA NA SALAMA WAPAMBA MOTO JIJINI DODOMA
Imewekwa: 23 May, 2023
UKAGUZI  WA NYAMA BORA NA SALAMA WAPAMBA MOTO JIJINI DODOMA

Maafisa Mifugo Kutoka Bodi ya Nyama Tanzania wakiongozwa na Ndg. Martin Mkindi wametoa onyo kali kwa Wafanyabiashara ya Nyama Mkoani Dodoma kusafirisha nyama bila ya kuzingatia hali ya usafi wa vifaa vya kubebea nyama hiyo.

Ndg. Mkindi amesema hayo Mei 2023, wakati wa ukaguzi wa Nyama Bora na Salama hususan ya Nguruwe katika Kata ya Ihumwa Jijini Dodoma. Ukaguzi huo umefanyika kufuatia usafirishaji holela wa nyama hiyo usiozingatia usafi na usalama.

Katika ukaguzi huo, wakaguzi kutoka Boi ya Nyama Tanzania walifanikiwa kuwakamata wafanyabiashara wa nyama ya Nguruwe wakisafirisha nyama Kutoka Machinjioni bila ya kujali usafi wa chombo cha Kubebea nyama hiyo.

. Aidha, Wakaguzi hao wamewasisitiza wafanyabiashara ya Nyama kuhakikisha Nyama wanayoipokea kutoka machinjioni inakuwa na muhuri wa Daktari aliyeikagua Nyama hiyo na kufuata sheria ya ufanyaji biashara a nyama ikiwemo kufanya usajili na kupata kibali cha kuenesha biashara hiyo kutoka Bodi ya Nyama Tanzania