NYAMA YA MBUZI YATEKETEZWA NA BODI YA NYAMA TANZANIA
Imewekwa: 29 May, 2023
NYAMA YA MBUZI YATEKETEZWA NA BODI YA NYAMA TANZANIA

Afisa Mkaguzi wa Bodi ya Nyama Bw. Geofrey Kakuru ameteketeza nyama ya mbuzi wapatao watano baada ya Nyama hiyo kugundulika kuwa si salama kwa matumizi ya Binadamu

Nyama hiyo imekamatwa mei, 2023 kwa ushirikiano na Jeshi la polisi na bodi ya nyama Tanzania ikiwa inasafirishwa kutoka msalato kwenda katika hotel ya rainbow iliyopo area “D” jijini Dodoma

“ Tumewakamata watu hawa kwa ushirikiano na jeshi la polisi kwa kuchinja mbuzi bila ya kukaguliwa na afisa mifugo, na pia jinsi wanavyo safirisha nyama hii si usafirishaji sahihi, hairuhusiwi klusafirisha nyama kwa kutumia pikipiki hilo ni kosa” amesema Bw. Kakuru

Wafanya biashara waliokamatwa wao wamekili kosa hilo la kuto fuata taratibu za uuzaji wa nyama

“Hatukufamu kama kufanya biashara ya nyama inaitaji kibali hata kama hauna bucha, tumekubali kulipa faini na kuanzia sasa tutafuata utaratibu wa kibali ili tufanye biashara yetu kwa uhuru” wamesema

Nae mmiliki wa hotel ya rainbow alioyekuwa anaenda kuuziwa nyama hiyo ameishukuru Bodi ya Nyama Tanzania kwa kukamata nyama hiyo japo amesisitiza kuwa huwa ananunua nyama yenye mhuri wa daktari wa mifugo kwa kuwa anajali sana afya za wateja wake

Bw. Kakuru amewasisitiza wanunuaji wa nyama na biodhaa zake wananunua nyama yenya muhuri halali na mbichi wa daktari wa mifugo kwani nyama hiyo itakuwa salama kwa matumizi ya binadamu