WANANCHI WAHIMIZWA KULA KUKU NA BIDHAA ZITOKANAZO NA KUKU
Imewekwa: 12 Oct, 2025
WANANCHI WAHIMIZWA KULA KUKU NA BIDHAA ZITOKANAZO NA KUKU

Washiriki wa maonesho ya kuku na ndege wafugwao wametakiwa kutumia maonesho hayo kuhimiza wananchi kula nyama ya kuku na bidhaa zitikanazo na nyama ya kuku kama vile soseji kutokana na ubora  na umuhimu wake katika lishe.

Hayo yamesemwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya nyama Tanzania Bw. John Chassama kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Abdul Mhinte alipokuwa akifunga maonesho ya tisa ya ndege wafugwao yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 10 hadi 11 Mlimani city jijini Dar es Salaam.

Msajili Chassama amesema “kupitia maonesho haya ulaji wa nyama ya kuku na mazao yake uhimizwe ili wananchi waweze kununua na kula kwani ni muhimu kwa afya”

Pia, Bw. Chassama alisisitiza wafugaji kuainisha kiasi cha  mahitaji ya nafaka kinachohitajika kwa ajili ya chakula cha mifugo ili kuwezesha upatikanaji wa chakula hicho kwa kushirikiana na mamlka zinazohusu chakula ikiwermo wizara ya kilimo.

Bw. Chassama aliendelea kuwasisitiza wafugaji wa ndege wafugwao kutumia elimu waliyopata katika mada mbalimbali zilizotolewa kwenye maonesho hayo kama chachu ya kuboresha uzalishaji wa mazao bora ya ufugaji.

Aidha, Bw. Chassama amewataka chama cha wafugaji kuhaklikisha kufikia Disemba 31, 2025 chama cha wafugaji kiwe kimesajiliwa na kutambulika rasmi kwani hii itawasaidia kuwezesha shughuli zao kirahisi ikiwemo kufikisha changamoto zao sehemu husika kama chama na kupatiwa ufumbuzi.

Awali akimnkaribisha Kaimuj Msajili Chassama kufunga maonesho hayo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo Bw. Costa Mrema ameishukuru serikali , washirikim wa maonesho na wahudhuriaji wa semina kwa kushirikiana na kufanikisha maonesho hayo kwa kiasi kikubwaambapo lengo ni kuyafanya bora zaidi kwa mwaka ujao.

Maonesho haya hufanyika kila mwaka na washiriki wamekuwa wakiongezeka kutoka mataifa mbalimbali. Ambapo kwa mwaka 2025 maonesho hayo yanafanyiuka kwa mara ya 9 huku Washiriki 53 kutoka ndani na nje ya nchi zikiwemo nchi za Malawi, Kenya, Afrika Kusini, India, Canada, Ujerumani na Ufaransa wameshiriki.