Bodi ya Nyama inawataka wafanyabiashara wa Nyama choma kupata usajili wa Bodi
Imewekwa: 21 Feb, 2023

USAJILI WA WAFANYABIASHARA YA NYAMA CHOMA NCHINI

Kwa mujibu wa sheria ya nyama namba 10 ya mwaka 2006 kifungu namba 17 na kifungu kidogo namba 1 hadi 3 kinamtaka kila mtu anayejishughulisha na biashara ya Mifugo, Nyama na mazao yake kuwa na cheti cha usajili kutoka Bodi ya nyama Tanzania. Kwa mujibu wa sheria tajwa hapo juu kila mfanyabiashara ya nyama choma nchini anapaswa kuwa na usajili ili kukidhi takwa la kisheria.