Dkt. Daniel Elias Mushi
Daniel Elias Mushi photo
Dkt. Daniel Elias Mushi
Msajili

Barua pepe: barua@tmb.go.tz

Simu: +255734295108

Wasifu

Dkt Daniel Elias Mushi ni mtaalamu wa Sayansi ya Nyama (Meat Science) mwenye shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka “Norwegian University of Life Sciences (NMBU), Norway. Aliteuliwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi kuwa Msajili wa Bodi ya Nyama kuanzia tarehe 1 April 2021. Kabla  ya uteuzi, amefanya kazi kama mhandhiri mwandamizi katika chuu Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).  Aidha, alipokuwa SUA amehudumu kama mwenyekiti wa kamati mbalimbali za kitaalam kama vile kamati ya Masomo ya Shahada ya kwanza (Undergraduate Studies Committee), kamati ya Utafiti na Machapisho (Research and Publication Committee) na hatimaye mwakilishi wa SUA na Mwenyekiti wa Kamati ya Shirika la  Viwango Nchini (TBS) inayohusika na uandaaji wa viwango vya nyama, kuku, mayai na mazao yake (Technical Committee for Meat, Poultry, Eggs and their Products  - AFDC 22). Dkt Mushi amefanya tafiti mbalimbali zilizofadhiliwa na washirika wa maendeleo kama NORAD, ASARECA, DANIDA na COSTECH ambapo ametoe machapisho ya kisayansi zaidi ya arobaini (40).