Ukaguzi

Ukaguzi wa Uzalishaji Mifugo, Nyama na Mazao yake

1.0 Lengo la Ukaguzi

Lengo la ukaguzi ni kuhakikisha wadau wa Tasnia ya Nyama nchini wanazingatia kanuni na miongozo ya uzalishaji ili kuzalisha nyama bora na salama kwa walaji.

1.1 Mkaguzi

Ni mtumishi aliyeteuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Nyama Na. 10 ya mwaka 2006 chini ya kanuni ya tisa (9) ya kupanga madaraja ya mifugo na chune (2010) kwa ajili ya kukagua eneo la kuzalisha mifugo (livestock production unit), minada ya mifugo, hati ya usajili, leseni, vitabu vya kumbukumbu na taarifa za kielektroniki zilizoko katika maeneo ya uzalishaji.

1.2 Maeneo ya Ukaguzi

 • Ukaguzi utafanywa katika maeneo yafuatayo:-
 • Ranchi
 • Wafugaji wa mifugo wa nyama wa aina zote kwa ajili ya biashara
 • Vyama vya wadau vinavyotambulika kisheria
 • Minada ya mifugo
 • Dalali wa Mifugo
 • Mwendesha Minada
 • Mfanyabiashara ya mifugo hai ndani na nje ya nchi, nyama (maduka ya Nyama) na mazao ya nyama
 • Wakala wa biashara ya nyama na mazao ya nyama
 • Watengenezaji na waagizaji wa mashine za uzalishaji wa nyama na pembejeo
 • Machinjio na Viwanda vya Nyama na bidhaa za Nyama
 • Waendesha matamasha ya Nyama
 • Waingizaji na wauzaji wa nyama ndani na nje ya nchi.

1.3 Utaratibu wa Ukaguzi

Utaratibu utakaofuatwa na Mkaguzi wakati wa kukagua utakuwa kama ifuatavyo;

 • Kufika katika eneo la ukaguzi na kujitambulisha kwa mmiliki wa eneo litakalokaguliwa
 • Kuwasiliana na mmiliki kwa njia ya kistaarabu, heshima na mamlaka
 • Kutoa maelezo ya kusudio la ujio wake
 • Kutumia njia za kidiplomasia, mbinu za ushawishi wa hali ya juu ili kupata taarifa za kina za eneo husika litakalokaguliwa
 • Kukagua eneo kulingana na vigezo vya ukaguzi
 • Kujadili matokeo ya ukaguzi na mmiliki, kuainisha mapungufu na kuelekeza namna ya kurekebisho mapungufu yaliyojitokeza