Imewekwa: 17 Oct, 2025
Bei ya wastani ya mifugo katika mnada wa Pugu imeshuka kwa wiki inayoishia tarehe 15 Oktoba 2025 ikilinganishwa na wiki iliyopita. Kwa kiasi kikubwa hali hiyo imesababishwa na kuongezeka kwa ugavi wa mifugo mnadani, huku uhitaji ukiwa ni mdogo.

