SERA YA FARAGHA Sera hii ya faragha inahusu Tovuti ya Bodi ya Nyama Tanzania na Taasisi yoyote ya kisheria inayosimamia, thibitisha au kutumia taarifa zinazoweza kupatikana kupitia tovuti hii. Mtumiaji anaweza kuingia kwenye tovuti hii bila kutoa taarifa zake binafsi. Hata hivyo, mtumiaji anakubali kutumia takwimu kwa kuzingatia sera ya faragha. Ikumbukwe kuwa tovuti hii inaweza kuwa imeunganishwa na kurasa nyingine, ambazo hazihusiani na sera hii ya faragha. Endapo mtumiaji ana swali lolote au hoja kuhusu sera hii ya faragha au faragha ya mtumiaji wakati anapotumia tovuti hii, anaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja kwa kutuma barua pepe kupitia anuani info@tmb.go.tz. Tovuti hii haikusudiwi kukusanya taarifa binafsi za watumiaji isipokuwa pale watembeleaji wanapoamua kutoa taarifa zao kwa hiari bila kulazimishwa. Baadhi ya taarifa zitakazopatikana kwa kutembelea kwako tovuti ya Bodi zinaweza kutunzwa ambazo ni pamoja na: Anuani ya barua pepe au tovuti uliyotumia kupakuwa tovuti ya Bodi ya Nyama Tanzania, tarehe na muda, jina la faili ulilotafuta na mada ulizoperuzi kwenye tovuti. Taarifa zilizokusanywa zitatumika kupata idadi ya wageni waliotembelea maeneo mbalimbali ya tovuti yetu na kutambua maeneo yenye changamoto. Pia tutatumia taarifa hizi kuboresha tovuti yetu na kuifanya iwe na manufaa. Tovuti ya Bodi ya Nyama Tanzania inaweza kutumia taarifa hizi kwa lengo la kufanya uchambuzi wa kitafiti. Taarifa binafsi hazikusanywi kwa sababu nyingine yoyote isipokuwa kufanyia kazi mahitaji yako. Taarifa zinazopatikana kupitia barua pepe yetu zitatumika tu kujibia hoja zako, na kusaidia kupata taarifa ulizoomba. Tutatoa taarifa hizi ulizotupatia kwa mdau mwingine wa Bodi ya Nyama Tanzania, endapo hoja zako zinaendana na hoja za mdau huyo au pale ilipoelekezwa kisheria.
S.L.P 1344 DODOMA,
Area D, Mtaa wa Ndugai,
Barabara ya Magufuli
Nukushi : Simu : +255734210199 Barua pepe : barua@tmb.go.tz
Copyright ©2017 Tanzania Meat Board . All rights reserved.
Designed and Developed by e-Government Authority (eGA). Inaendeshwa na TMB.