BODI YA NYAMA TANZANIA(TMB)
TANGAZO KWA UMMA
“KATAZO LA MATUMIZI YA MAGOGO, NONDO ZENYE KUSHIKA KUTU NA DAWA YA MBU KATIKA MADUYA KUUZA NYAMA”
Bodi ya Nyama Tanzania inapenda kuwajuza wamiliki wa maduka ya kuuza Nyama (mabucha) na umma wa Watanzania kwa ujumla kuwa,mabucha yote yanatakiwa Kutumia misumeno ya kisasa kukatia Nyama,nondo za aluminium kuning'inizia Nyama na majokofu wakati wa kutoa huduma kwa walaji.Aidha bucha zinatakiwa kuwa katika usafi ikiwemo kuwa na wavu wa kioo ilikuzuia uingiaji wa wadudu Warukao buchani na sio kutumia dawa ya mbu katika kuua wadudu hao.Pia,wauzaji wote Wa nyama mabuchani wanatakiwa kupima afya kila baada ya miezi sita,kuvaa Mabuti meupe na makoti meupe wakati wote wa kuuza nyama. kutumia magogo,nondo zenye kushika kutu,dawa ya mbu, kutopima afya na kutovalia mavazi maalumu ni kosa kisheria, n aadhabu yake kwa kila kosa ni kifungo kisichozidi miezi minne au faini isiyo pungua laki moja au vyote Kwa pamoja,
kifungo na faini Wananchi wanasisitizwa kuepuka kununua Nyama kwenyemabucha yote yasiyokuwa nasifahizi.
Tafadhali,toa taarifa juu ya uwepo wa bucha linalokiuka tararibu hizi kwa kuwasiliana na Bodi ya NyamaTanzania kupitia barua pepe barua@tmb.qo.tz au kwa kupiga simu Nambari 0734996218 au kwa kuwasilisha taarifa katika ofisi za kanda za Bodi ya Nyama zilizopo Arusha Mwanza,Tabora,Dar-es-salaam na Mbeya au kwa kuwasiliana na Afisa mifugo aliye karibu nawe.
Bodi itaendelea na ukaguzi wa mabucha mara zote ilikuwabaini wale wote wanao hatarisha afya za walaji kwa kukiuka taratabu hizi na kuwachukulia hatua kwa Mujibu wa sheria
IMETOLEWA NA OFISI YA MSAJILI,
BODI YA NYAMA TANZANIA,
DODOMA,
TAREHE 26 JULAI,2022.
S.L.P 1344 DODOMA,
Area D, Mtaa wa Ndugai,
Barabara ya Magufuli
Nukushi : Simu : +255734210199 Barua pepe : barua@tmb.go.tz
Copyright ©2017 Tanzania Meat Board . All rights reserved.
Designed and Developed by e-Government Authority (eGA). Inaendeshwa na TMB.